Wakristo waadhimisha sikukuu ya Ijumaa kuu

  • | Citizen TV
    885 views

    Viongozi wa dini ya kikristu nchini Wamewataka maafisa wakuu wa serikali wanaoongoza kamati ya mazungumzo inayotafuta suluhu ya mgomo wa madaktari, baraza la magavana, pamoja na viongozi wa chama cha madaktari kutafuta mwafaka huku mgomo huo ukiingia siku ya kumi na sita. Kwenye maadhimisho ya sikukuu ya ijumaa kuu katika kaunti ya Mombasa, Askofu mkuu wa kanisa katoliki Martin Kivuva amesikitikia mahangaiko ya wagonjwa huku pande hizo mbili zikishikilia misimamo mikali.