Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Francis Ogolla Afariki katika Ajali ya Ndege

  • | VOA Swahili
    995 views
    Rais wa Kenya William Ruto Alhamisi jioni alitangaza kifo cha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Francis Ogolla, kilichotokana na ajali ya helikopta iliyotokea majira ya alasiri Kaskazini Magharibi mwa nchi. Akihutubia wanahabari katika ikulu ya Nairobi, Ruto alisema kuwa ndege hiyo ya kijeshi ilianguka eneo la Sindar kaunti ya Elgeyo Marakwet mwendo wa saa nane na dakika 20 alasiri. Ruto alisema watu wengine 9 pia walifariki katika ajali hiyo na kuongeza kwamba maafisa wengine wawili waliokuwa kwenye ndege hiyo walinusurika na wanaendelea kupatiwa matibabu hospitalini. Tisa hao ni pamoja na Brigedia Swale Saidi, Kanali Duncan Keittany, Luteni Kanali David Sawe, Meja George Benson Magondu, Kapteni Sora Mohamed, Kapteni Hillary Litali, Sajenti Mwandamizi John Kinyua Mureithi, Sajenti Cliphonce Omondi, na Sajenti Rose Nyawira. "Nina huzuni kubwa kutangaza kwamba Jenerali Francis Omondi Ogolla, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Kenya, amefariki” Rais Ruto alisema. Katika taarifa yake, Ruto alisema Ogolla aliondoka Nairobi Alhamisi asubuhi kuelekea kazini katika eneo la Bonde la Ufa, ambako alikagua ukarabati wa shule tano Elgeyo Marakwet. Pia alikuwa Turkana ambapo alikutana na kuzungumza na wanajeshi waliotumwa huko kabla ya kwenda Pokot Magharibi. Wakati wa ajali hii, Jenerali Ogolla na timu yake walikuwa wakielekea Kaunti ya Uasin Gishu. Kufuatia kifo cha Ogolla, Ruto ametangaza siku tatu za maombolezo huku bendera zikipepea nusu mlingoti. "Wakati huu wa maombolezo ya kitaifa, bendera ya Kenya, Bendera ya Jeshi la Ulinzi la Kenya, na bendera ya jumuiya ya Afrika Mashariki zitapepea nusu mlingoti katika balozi za Jamhuri ya Kenya na Kenya nje ya nchi," Ruto alisema. Uchunguzi umeanza kubaini kilichosababisha ajali hiyo. #mkuuwamajeshi #Jenerali #FrancisOgolla #rais #kenya #williamruto #ndege #jeshi #ajali #nairobi #voa #voaswahili
  • 15 Jul 2025 - Mugithi star and serving police officer Samuel Muchoki, widely known as Samidoh, has confirmed his long‑awaited return to
  • 15 Jul 2025 - Inclusive National Justice, Economic & Civic Transformation (INJECT) Party leader Morara Kebasohas issued a candid warning to Kenyans,
  • 15 Jul 2025 - A Senate committee has recommended an amendment to the County Government Act to provide for the recall of nominated Members of County Assemblies (MCAs).   The Senate Justice and Legal Affairs Committee further wants the amendments to clearly outline the…
  • 15 Jul 2025 - Spanish police have arrested nine people over rare anti-migrant unrest that rocked the town of Torre Pacheco, authorities said on Monday.
  • 15 Jul 2025 - People’s Liberation Party (PLP) leader Martha Karua has clarified the reasons for travelling to the United States of
  • 15 Jul 2025 - Standard Chartered has projected a weakening of the US dollar over the next six to 12 months, a development that could ease Kenya’s inflation and unlock new investment opportunities as investors seek yields outside the US.  As a result, Kenya’s…
  • 15 Jul 2025 - Busia Senator Okiya Omtatah has called for the resignation of President William Ruto and Interior Cabinet Secretary Kipchumba
  • 15 Jul 2025 - He struggles with political correctness and can barely disguise his impatience.  He easily veers off script and remains untamed through the interview to the delight of press corps.   The technocrat in him is fast fading.  Former Interior Cabinet…
  • 15 Jul 2025 - A nighttime fire at a nursing home has left nine people dead in the northeastern US state of Massachusetts after a desperate rescue operation, local authorities said Monday.
  • 15 Jul 2025 - The Democratic Action Party-Kenya (DAP-K) party leader, Eugene Wamalwa, has disclosed that the United Opposition will front one presidential candidate