Ibada ya wafu ya wanahewa 6 waliofariki kwenye ajali ya ndege yaandaliwa

  • | KBC Video
    205 views

    Ibada ya wafu ya wanajeshi sita waliofariki kufuatia ajali ya ndege juma lililopita iliandaliwa leo kwenye kambi ya wanahewa ya Moi katika mtaa wa Eastleigh, jijini Nairobi. Kamanda wa jeshi la wanahewa Meja Jenerali John Omenda aliyewaongoza wanajeshi wenzake kutoa heshima za mwisho kwa wenzao walioangamia alieleza imani kuwa kundi la wataalamu wanaochunguza ajali hiyo ambayo pia ilisababisha kifo cha mkuu wa majeshi jenerali Francis Ogolla watapata jawabu hivi karibuni.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive