Mswada wa fedha 2024 wapendekeza ushuru wa asilimia 16 kwa mkate

  • | Citizen TV
    827 views

    Bunge la kitaifa linatarajiwa kurejelea vikao vyake kwa kuandaa vikao maalum kujadili mswada wa fedha wa mwaka 2024. Vikao hivi vikitarajiwa kuangazia yaliyomo kwenye mswada huu ulioratibu kwa mapana mzigo zaidi wa ushuru kwa wakenya. Mbali na kupendekeza ushuru zaidi utakaopandisha bei ya mkate na hata ushuru wa kila mwaka wa gari, mswada huu pia unapendekeza kuondolewa kwa afua ya ushuru kwa huduma za benki na ushuru zaidi kwa bodaboda