Waathiriwa wa maporomoko ya ardhi Mathioya wasajiliwa ili kupewa stakabadhi muhimu upya

  • | Citizen TV
    324 views

    Waathriwa wa maporomoko ya ardhi pamoja na wakazi wa Ngutu huko Mathioya kaunti ya Murang'a wamepelekewa huduma za kurejeshewa stakabadhi muhimu walizopoteza kama vitambulisho na vyeti vya kuzaliwa. Zoezi hili liliongozwa na afisa mkuu wa shirika la Ahadi Kenya daktari Stanley Kamau chini ya shirika la HUDUMA MASHINANI. Kamau aliwasihi jamaa za waliofurushwa kwao na mvua au maporomoko ya ardhi kuwapa hifadhi ya muda wakati wanaendelea kujenga makao mapya. Kamau alikuwa akizungumza na waathiriwa maporomoko yaliyouwa watu sita mwezi Aprili katika shule ya msingi ya Ngutu.