Wakulima Trans Nzoia wataka walipwe fidia ya mbolea ghushi

  • | Citizen TV
    207 views

    Wakulima ambao hawajapokea mbolea ya kutandaza wanaitaka serikali kuwalipa fidia kwa hasara wanaotazamia kwa madai kuwa mavuno ya mwaka huu yatapungua. Wakulima hao kutoka kaunti ya Trans Nzoia wanasema kuwa waliathirika na mbolea ghushi wakati wa upanzi na hadi sasa hawajapata kunyunyizia mahindi yao mbolea ya kutandaza kwani mbolea hiyo hazipatikani. Sasa wanasema iwapo mbolea hio itazidi kuchelewa, mimea yao itafifia mashambani. Katibu katika wizara ya kilimo paul rono anasema mbolea hiyo itawafikia wakulima katika muda wa wiki mbili zijazo.