Nyumba kadhaa zilizo karibu na mito zabomolewa Shauri Moyo na Blue Estate

  • | KBC Video
    24 views

    Waziri wa usalama wa taifa Profesa Kithure Kindiki amesema sababu hasa ya kuwahamisha watu kutoka kingo za mito ni kwa ajili ya usalama wao. Akiongea alipozuru mitaa ya mabanda ya Mathare, Kiamaiko na Mukuru kwa Reuben katika kaunti ya Nairobi, Profesa Kindiki aliwapongeza wananchi kwa ushirikiano wao katika shughuli hiyo. Alibainisha kuwa kuna haja ya kulinda kingo za mito ya Nairobi pamoja na maisha ya wale walioathiriwa na mafuriko ya hivi majuzi. Familia elfu-40 zilizojumuisha watu elfu-181 zimehama kwa hiari kutoka kwa hifadhi za mito ya Nairobi, Mathare na Ngong na chemi chemi zingine za mito ya Nairobi.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive