Baadhi ya viongozi wa Rift Valley wametetea uhusiano wa rais Ruto na naibu wake

  • | KBC Video
    40 views

    Baadhi ya viongozi wa eneo la Rift Valley wametetea uhusiano wa kikazi baina ya rais William Ruto na naibu rais Rigathi Gachagua na kukosoa wapinzani wao wa kisiasa kwa kuchochea mgawanyiko baina ya viongozi hao wawili. Viongozi wa mrengo wa Kenya Kwanza walioandamana na naibu rais Rigathi Gachagua kwa ibada ya Jumapili katika shule ya msingi ya Matharu, katika eneo bunge la Kesses, kaunti ya Uasin Gishu, walitoa wito kwa viongozi wengine katika mrengo huo tawala kukomesha na kujiepusha na siasa za urithi za mwaka-2032. Kwa upande wake, naibu rais alitoa wito wa kusitishwa kwa siasa za kikabila ambazo alisema awali zilisababisha migawanyiko katika taifa hili.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive