Joho amewahakikishia wanachama wa ODM uwazi uchaguzini

  • | Citizen TV
    1,543 views

    Naibu Kinara wa chama Cha ODM Hassan Joho amehakikishia wanachama kuwa watazingatia mbinu mwafaka zenye usawa katika uchaguzi wa chama. Akizungumza katika kaunti ndogo ya Nyatike Kaunti ya Migori wakati wa mkutano ulioleta pamoja viongozi na wanachama, Joho alieleza kuwa Nia ya chama ni Kumaliza migogoro ambayo huibuka baada ya uchaguzi. Joho alieleza kuwa watahusisha wanachama wote Ili kufikia uamuzi mwafaka na kuleta suluhu ya kudumu kabla na baada ya uchaguzi huo. Viongozi wa chama walielezea umuhimu wa utangamano na kuheshimu mikakati ya chama na kukashifu vikali mapendekezo ya Mswada wa fedha wakieleza kuwa itaongeza gharama Kwa wananchi.