Wenyeji wa Bundalangi wahofia Kipindupindu

  • | Citizen TV
    70 views

    Huku wahanga wa mafuriko kutoka kwa familia zaidi ya 7000 wakisalia kambini kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa, uwezekano wa mkurupuko wa magonjwa yanayosababishwa na maji chafu kama vile kipindupindu unawatia kiwewe wakazi, viongozi pamoja na maafisa kutoka shirika la msalaba mwekundu huku busia. Maafisa kutoka shirika la msalaba mwekundu sasa wameanzisha mikakati ya dharura ya kuhamasisha wahanga hao katika kambi na majumbani umuhimu wa kuzingatia usafi katika juhudi za kuzuia msambao wa magonjwa.