Hamasisho kuhusu hedhi

  • | Citizen TV
    108 views

    Kundi la vijana la kutetea haki za kibinaadamu kutoka kaunti za pwani zikiwemo mombasa, kilifi na Taita-Taveta limeanzisha mradi wa kuinua viwango vya elimu vya mtoto wa kike eneo la kishushe kaunti ya Taita Taveta. kundi hilo limetoa sodo za hedhi na mafunzo ya afya na usafi wa hedhi katika shule tofauti eneo hilo ili kupambana na changamoto ya idadi kubwa ya wasichana wanaokosa kuhudhuria masomo kutokana na ugumu wa upatikanaji wa sodo.