Skip to main content
Skip to main content

Mwanamme afariki kwenye mahakama ya Bungoma akisubiri kusikilizwa kwa kesi yake

  • | KBC Video
    2,326 views
    Duration: 2:38
    Taharuki ilitanda katika Mahakama ya Bungoma baada ya mzee mmoja aliyekuwa akisubiri kusikilizwa kwa kesi ya mzozo wa ardhi kufariki nje ya mahakama hiyo. Idara ya Mahakama imesema kuwa marehemu aliwasili mahakamani akionekana kuwa katika hali mbaya ya kiafya, na kesi yake ikapewa kipaumbele kusikilizwa. Hata hivyo, aliamua kupumzika nje ya mahakama akimsubiri wakili wake lakini baadaye akapatikana bila fahamu. Polisi walithibitisha kifo chake muda mfupi baadaye. Kaka yake marehemu amesema kuwa alikuwa anaugua maradhi ya moyo. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive