Watetezi wa haki za kibinadamu Bungoma walalamikia ubakaji

  • | Citizen TV
    220 views

    Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu Katika kaunti ya Bungoma Sasa yanamtaka jaji mkuu Martha koome na kamishna wa masuala ya haki na sheria nchini kuingilia Kati na kuhakikisha waathiriwa wa dhulma za kijinsia wanapata haki.Wakizungumza mjini Bungoma wanaharakati wa mashirika hayo wanadai kumekuwa na utepetevu katika kesi za unajisi huku wahalifu wakidaiwa kuachiliwa huru na kuhatarisha jamii.