Wakaazi wa kigumo waunganishwa na nguvu za umeme

  • | Citizen TV
    192 views

    Wakaazi wa Rugongo Ruraya katika eneo bunge la Kigumo kaunti ya Murang’a wana kila sababu ya kutabasamu baada ya kuunganishwa na nguvu za umeme. Zaidi ya wakaazi 6,000 wanatazamiwa kupata umeme katika Kaunti ya Murang’a kufuatia kutekelezwa kwa miradi 87 ya usambazaji wa umeme na Shirika la Umeme Vijijini (REREC). Miradi, ambayo iko katika hatua tofauti za utekelezaji ina gharamu jumla ya shilingi Milioni 434. 70% ya wakaazi eneo la kigumo wana umeme.