Mnara wa kuwakumbuka viongozi waliofariki kwenye ajali ya ndege miaka 18 iliyopita huko Marsabit

  • | Citizen TV
    88 views

    Baraza la kitaifa kuhusu mashujaa limetangaza mpango wa kuweka mnara wa kuwakumbuka wakenya 14 waliofariki katika mkasa wa ajali ya ndege miaka 18 iliyopita katika kaunti ya Marsabit. 14 hao akiwemo waziri wa leba marehemu ahmed khalif na wabunge sita walifariki wakielekea katika mkutano wa amani katika eneo hilo. Baraza hilo limesema ujenzi wa mnara huo utakuwa wa kuwakumbuka mashujaa hao na kuhimiza amani miongoni mwa jamii zinazoishi maeneo hayo. Maafisa wakuu wa baraza hilo, viongozi na wakazi waliozuru eneo la tukio wamehimiza uwiano na umoja.