- 383 viewsDuration: 3:11Watu watatu zaidi wanaendelea kutibiwa kutokana na ugonjwa wa kipindupindu eneo la Kilgoris, Transmara, kutokana na ugonjwa wa kipindupindu, uliowaua watu watano kufikia sasa. Wakaazi wa baadhi ya maeneo yaliyoathirika kama vile kitongoji cha Majengo na Huruma sasa wakiitaka serikali kuingilia kati hali chafu ya mazingira, wanayosema inazidi kusambaza kipindupindu hiki kilichowaathiri zaidi ya watu 50 kufikia sasa.