Wakazi wa Samburu wahimizwa kupanda miti kama njia ya kuhifadhi mazingira

  • | KBC Video
    7 views

    Wakazi wa kaunti ya Samburu wametakiwa kukumbatia suala la upanzi wa miti na kutunza misitu na vyanzio vya maji kama njia ya kuhifadhi mazingira. Hayo ni kwa mujibu wa mwana-harakati wa mazingira Susan Boit ambaye alisema kuwa azma yao ni kutimiza ndoto ya rais William Ruto ya kupanda miti bilioni-15 katika kipindi cha miaka kumi ijayo. Akizungumza katika msitu wa Kirisia wakati wa hafla ya upanzi wa miti, Boit alisema kuwa kufikia sasa miche milioni-300 ya miti imepandwa kote nchini kati ya mwezi Disemba 2022 na Juni 2024. Kuhusu suala la marufuku ya kulisha mifugo kwenye misitu,Boit aliridhia kauli ya waziri wa Mazingira Soipan Tuiya kuwa wafugaji hawapaswi kupeleka mifugo misituni. Boit alisema marufuku hiyo inanuiwa kuhifadhi miti changa inayopandwa ili ipate nafasi ya kukua. Hata hivyo, kamati ya kiufundi iliyoundwa na serikali inaratibu mikakati kuhusu jinsi wafugaji wanaweza kulisha mifugo katika misitu.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive