Masaibu ya wanahabari:Chama cha KUJ chatoa ilani ya mgomo

  • | KBC Video
    7 views

    Chama cha wanahabari humu nchini Kenya kimetoa ilani ya mgomo ya siku 14 kwa waziri wa Leba Florence Bore kutokana na kile kilichotajwa kuwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu katika kampuni ya Standard Group. Akihutubia wanahabari jijini Nairobi katibu mkuu wa chama cha wana-habari-KUJ, Erick Oduor alisema wafanyikazi katika kampuni hiyo wamekosa mshahara kwa miezi saba licha ya hali ngumu ya kiuchumi inayoshuhudiwa humu nchini. Aidha alisikitika kuwa huenda wafanyakazi hao wakapoteza mamilioni ya pesa walizowekeza katika chama chao cha ushirika kwani mwajiri wao hajawasilisha michango hiyo kwa chama hicho.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive