Bodi ya kiwanda cha toror yamtaka john chebochok kujiuzulu

  • | Citizen TV
    785 views

    Shinikizo la wanunuzi wa chai wa kimataifa limeilazimisha Bodi ya Usimamizi wa kiwanda cha chai cha Toror kumwomba John Chebochok ajiuzulu kama mkurugenzi wa Kiwanda hicho. Baada ya kikao kirefu cha faragha katika Kiwanda cha Chai cha Toror, Mwenyekiti wa Bodi hiyo Japheth Chepkwony alisema kuwa Chebochok bado hajatangazwa kuwa mkurugenzi. Aliwahakikishia wanunuzi wa chai kuwa licha ya utata uliozingira uchaguzi wa Chebochok, usindikaji wa chai katika Kiwanda hicho unaendelea kukidhi viwango vinazohitajika.Chebochok, mkandarasi wa zamani wa Finlays, anadai kuwadhulumu wanawake kingono.