Rais atangaza siku sita za mazungumzo kuanzia Jumatatu

  • | K24 Video
    96 views

    Rais William Ruto na kinara wa Azimio Raila Odinga wamekubaliana kuandaa kongamano la siku sita litakalowaleta pamoja wadau kutoka sekta mbalimbali pamoja na vijana ili kushiriki mazungumzo ya kitaifa na kutafuta suluhu ya kudumu ya masuala muhimu yanayowakumba wakenya. Hata hivyo tangazo hilo limeibua hisia mseto kutoka kwa vijana mitandaoni huku wakimkejeli Raila Odinga kwa kuhusika katika mchakato huo wakidai kuwa analenga kujinufaisha binafsi.