Vuguvugu la Gen Z latingisha upinzani

  • | K24 Video
    211 views

    Runinga ya K24 imebaini kuwa kuna mengi yaliyojadiliwa katika kikao cha jana kati ya serikali na baadhi ya viongozi wa upinzani ambayo viongozi wenyewe hawakuyaweka wazi. Siasa za nipe nikupe zilijadiliwa katika kikao cha faragha kilichoandaliwa kabla ya taarifa ya pamoja ya viongozi hao. Baadhi ya viongozi wameiarifu K24 kuwa upinzani uliahidiwa nafasi nne kuu katika serikali ya kenya kwanza kama njia mojawapo ya kutuliza joto la siasa. Haya yanajiri huku viongozi tofauti wa upinzani wakitoa taarifa kinzani kuhusu mazungumzo ya mustakabali wa taifa