Mpigambizi Maria Brunlehner aimarisha matayarisho kwa Olimpiki

  • | Citizen TV
    249 views

    Mpigambizi wa Kenya Maria Brunlehner anaendeleza mazoezi yake jijini miramas tayari kwa michezo ya olimpiki itakayoanza baadaye mwezi huu. Maria mwenye makazi yake nchini marekani, atakuwa mkenya wa pekee kwenye uogeleaji upande wa wasichana akitarajiwa kushiriki kwenye shindano la mita 50. Mkenya mwengine ambaye atajiunga nae kwenye maandalizi ni ridhwan abubakar ambaye atapeperusha bendera ya kenya kwenye shindano la mita mia nne kwa wavulana. Timu za kenya zinaendelea kuwasili kambini miramas kwa maandalizi ambapo tayari timu ya raga na ile ya voliboli zilikuwa za kwanza kufika.