- 380 viewsRais wa zamani wa Marekani Donald Trump amesema Seneta wa Ohio James David Vance (JD) Vance, mwenye umri wa miaka 39, ndiye chaguo lake la mgombea mwenza kuelekea uchaguzi wa mwezi Novemba. Trump alisema kupitia ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa Truth Social: “Baada ya kutafakari na kufikiria kwa muda mrefu, na kwa kuzingatia vipaji vya hali ya juu vya wengine wengi, nimeamua kwamba mtu anayefaa zaidi kushika wadhifa huop ni JD Vance wa jimbo la Ohio." Kongamano la Kitaifa la Chama cha Republican lilianza wiki hii, huku wajumbe na maafisa wakiwasili mjini Milwaukee, Wisconsin wakati kukiwa na msukosuko uliofuatia jaribio la kumuua Trump Jumamosi. Trump anatarajiwa kuteuliwa rasmi kuwa mgombea urais kwa tikiti ya chama cha Republikan. Shirika la habari la AFP linaripoti kuwa kupanda kwa J.D. Vance hadi mgombea mwenza wa Donald Trump kunakamilisha mabadiliko makubwa kwa seneta huyo, ambaye sasa anaonekana kuwa sura ya baadaye ya chama cha Republican. Vance amekuwa mmoja wa watatezi wakubwa wa Trump katika bunge, akiunga mkono sera mbalimbali zenye utata kama vile kupinga uhamiaji, kusisitiza Ukristo kama njia ya kukuza maadili ya umma na ya kibinafsi, na kupinga vita vya Ukraine dhidi ya uvamizi wa Russia. Mapema mwaka huu, seneta huyo wa Ohio alionya wale ambao hawamuungi mkono Trump kwamba "ana kumbukumbu ya muda mrefu." "Kama unampinga Trump na wale anaowaunga mkono, usitegemee msaada wangu," alisema. Hata hivyo, Vance katika siku za nyuma alikuwa mkosoaji wa Trump, na wakati mmoja alimuita "Hitler wa Marekani," kwa mujibu wa shirika la habari la AFP. #donaldtrump #marekani #republikan #chama #jdvance #jimbo #ohio #milwaukee #wisconsin #raiswazamani
Trump amteua Seneta JD Vance kuwa mgombea mwenza
- - Duniani Leo ››
- - Kenya-Finland Ties ››
- 14 May 2025 - Presidential aspirants are focusing on the youth, as the 2027 general election battle shapes up.
- 14 May 2025 - The government last week unveiled its leasing programme, handing over four public sugar factories to private players.
- 14 May 2025 - The report highlights how employers subjected the women to extreme exploitation in private homes, often fuelled by racism.
- 14 May 2025 - NLC boss admitted that while the commission can investigate land grabs, it lacks authority to revoke illegal titles.
- 14 May 2025 - Chairman Anangwe says the varsity should be allowed to function without threats.
- 14 May 2025 - The audit found that ministries, departments and agencies failed to provide documentation for Sh783.9 million in spending.
- 14 May 2025 - The commission said they need Sh3 billion to hire the interns on permanent and pensionable terms.
- 14 May 2025 - Safaricom CEO Peter Ndegwa has addressed concerns about the company's involvement in the Social Health Authority (SHA) system, clarifying that its role is limited to the digitisation of the process.
- 14 May 2025 - Sean "Diddy" Combs' former girlfriend, Casandra Ventura, the star prosecution witness at the hip-hop mogul's sex trafficking trial, testified on Tuesday that her music career began to suffer as she increasingly spent her time participating in days of…
- 14 May 2025 - Senators yesterday put Kericho Governor Dr Eric Mutai on the spot over stalled Early Childhood Development and Education (ECDE) classroom projects, some of which have remained incomplete since the onset of devolution. This even as the lawmakers…