IPOA yasema polisi wanawanyima taarifa

  • | Citizen TV
    5,203 views

    Tume ya kutathmini utendakazi wa polisi sasa inasema kuwa maafisa wa polisi wanaihangaisha na kuhujumu uchunguzi wao kuhusiana na tuhuma za ukatili na mauaji zinazowakabili maafisa wa usalama wakati wa maandamano. Ipoa inasema kuwa usimamizi wa polisi umewanyima habari kuhusu maafisa waliotumwa kwenye maeneo ambako visa vya kutumia nguvu kupita kiasi vimeripotiwa na silaha zilizokuwa mikononi mwao .