Jinsi hatari kubwa imeendelea kuwakodolea macho wakaazi wanaotumia daraja la Loresho-Kangemi

  • | Citizen TV
    1,939 views

    Hatari kubwa imeendelea kuwakodolea macho wakaazi wanaotumia daraja linalounganisha eneo la Loresho na soko la Kangemi kwenye barabara kuu ya Waiyaki. Hii ni kwa kuwa daraja hilo halijakamilika tangu lilipoanza kujengwa zaidi ya miaka miwili iliyopita. Wanafunzi na hata wahudumu wa soko hilo wakihatarisha maisha kila siku wanapovuka, huku wengine wakiendelea kuuguza majeraha. Mwanahabari Givens Chanzu ameandaa taarifa ifuatayo