Harakati za kuimarisha matokeo katika shule za upili,

  • | K24 Video
    20 views

    Katika harakati za kuimarisha matokeo katika shule za upili, wanafunzi wa vyuo vikuu na wasomi wameanza mchakato wa kutoa ushauri nasaha kwa wanafunzi katika shule zinazopata alama ya chini ya C mashariki mwa kenya. Wasomi hao wanasema mafunzo hayo ni kichocheo cha wanafunzi kuandikisha matokeo mazuri katika mtihani wa KCSE mwaka huu. Shule tatu nne kutoka kaunti ya machakos na zengine kutoka kaunti za kitui na makueni zimefaidi na mafunzo ya jana.