Mashirika 16 ya kijamii yanachunguzwa na DCI

  • | Citizen TV
    1,495 views

    Mamlaka ya kudhibiti mashirika yasiyo ya serikali na ya kijamii imewasilisha faili za mashirika 16 kwa idara ya upelelezi wa jinai (DCI) kwa uchunguzi kuhusiana na ufadhili wa maandamano ya vijana. Mamlaka hiyo inasema kuwa kati ya mashirika 16 yaliyopata fedha kutoka kwa wakfu wa Ford Foundation, ni matatu tu ambayo yamesajiliwa humu nchini. Hatua hiyo inajiri baada ya katibu katika wizara ya mambo ya kigeni, korir sing'oei, kuandikia barua wakfu wa Ford akidai kuwa unafadhili maandamano.