Equity Duma imemaliza nafasi ya tatu kwenye ligi kuu ya mpira wa kikapu

  • | Citizen TV
    200 views

    Timu ya Equity Dumas imemaliza kwenye nafasi ya tatu kwenye ligi kuu ya mpira wa kikapu nchini wakiilaza Strathmore Blades 71-66 uwanjani Nyayo. Wanabenki hao waliopoteza mechi zote za nusu fainali dhidi ya mabingwa Thunder, walianza vyema na kushinda robo ya kwanza 22-20 na kufuatia ya pili kwa 15-13. Equity iliendeleza ubabe wake kwa kushinda robo ya tatu na nne kwa vikapu 20-13 na 20-14 mtawalia. Upande wa wasichana Zetech Sparks iliwazidi Strathmore Swords 46-40 na kumaliza nafasi ya tatu.