Wajumbe wa ODM wataka mabadiliko bora ya uongozi

  • | Citizen TV
    1,378 views

    Wajumbe wa chama cha ODM sasa wanataka mabadiliko katika chama hicho huku wakimtaka kinara wa chama hicho Raila Odinga kuwateuwa viongozi wachanga kuongoza chama hicho. Wajumbe hao kutoka eneo la Magharibi na Nyanza wamepigia debe gavana wa Kisii Simba Arati kuwa naibu kinara wa chama cha ODM. Katika mkutano uliofanyika kaunti ya Kisumu, wamemataka gavana Arati kupiga jeki umaarufu wa chama iwapo ataidhinishwa. Kwingineko katika kaunti ya Nairobi kundi jingine la akina mama limewataka wajumbe kumpa nafasi hiyo gavana wa Homa Bay Gladys Wanga.