- 463 viewsDuration: 2:32Miungano ya wahadhiri na wafanyakazi wa vyuo vikuu nchini imesisitiza kuwa mgomo wao wa kitaifa utaendelea. Mgomo huu umeingia siku yake ya 28 leo huku mazungumzo ya kutatua mgomo huo kati yao na serikali yakionekana kukosa muafaka. Awali waziri wa elimu Julius Ogamba alielezea matumaini kuwa wataafikiana, ila chama cha UASU kimeshikilia kuwa ni lazima walipwe shilingi bilioni 7.9 wanazodai