Maafisa watano wanaozuiliwa kwa tuhuma za kuhusika na kutoroka kwa mahabusu 13 kujua hatma yao leo

  • | Citizen TV
    1,231 views

    Huku maafisa watano wanaozuiliwa kwa tuhuma za kuhusika na kutoroka kwa mahabusu 13 kutoka kwenye seli za kituo cha polisi cha Gigiri wakisubiri kujua hatma yao, Sasa imebainika kuwa mahabusu hao walitoka wakitumia mlango wa kituo hicho. kinyume na ilivyodhaniwa kwamba washukiwa hao walikata waya unaozingira seli na kupanda juu ya paa ya kituo hicho, washukiwa hao walifunguliwa seli na kuondoka bila kukata jasho