Mikakati ya kuzuia ufadhili yapendekezwa

  • | KBC Video
    33 views

    Mshauri wa maswala ya usalama wa taifa Monica Juma ameelezea mpango wenye vipengele vitano wa kuzuia mashirika ya kigaidi kupata fedha na kwa hivyo kupunguza uwezo wao na kudhibiti shughuli zao. Haya yamefichuliwa huku wasimamizi wakuu wa sera na watoa maamuzi katika sekta ya kukabiliana na ugaidi kutoka mataifa manane ya bara la Afrika wakikusanyika jijini Nairobi. Mkutano huo wa siku moja chini ya kauli-mbiu "Kukabiliana na Ufadhili wa Ugaidi" ulizingatia mikakati ya kugundua na kukabiliana na ongezeko la mitandao ya kifedha ya magaidi kupitia mbinu za kawaida na za mtandaoni ambazo huwawezesha kukusanya, kuhamisha, kuhifadhi na kutakasa fedha ili kufanikisha shughuli zao.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive