Maambukizi mapya ya ukimwi yaongezeka Migori

  • | KBC Video
    43 views

    Wadau wa sekta ya afya katika kaunti ya Migori wameelezea wasiwasi kuhusu maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi katika eneo hilo. Kwa mujibu wa naibu mshirikishi wa masuala ya ujana katika kaunti hiyo, Faith Osian, maambukizi hayo mapya yanahusisha zaidi vijana waliobaleghe.Wadau hao sasa wametoa wito wa kuendelea kampeni miongoni mwa vijana wa umri wa kati ya miaka-10 na 19 kuhusu ndoa za mapema, maambukizi ya ukimwi na dhuluma za kijinsia. Ushirikishaji vijana katika michezo pia umetajwa kuwa jukwaa la kuwashauri vijana kuhusu maovu ya kijamii kama vile maambukizi ya Ukimwi.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive