Katiba mpya ya Kenya yaadhimisha miaka 14

  • | KBC Video
    27 views

    Huku Kenya ikiadhimisha miaka 14 tangu kuratibiwa kwa katiba mwaka 2010 wadau wakiwemo chama cha wanasheria nchini, makundi ya kidini na mashirika ya kijamii yameonya dhidi ya majaribio ya wanasiasa ya kurekebisha sheria hiyo kwa manufaa ya kibinafsi. Walishtumu mpango wa NADCO uliopendekeza kujumuishwa kwa afisi mpya zikiwemo afisi ya kiongozi rasmi wa upinzani na waziri mkuu wakisema kuwa mabadiliko yoyote kwenye katiba yanafaa kuwa kwa manufaa ya wananchi. Na jinsi mwanahabari wetu Giverson Maina anavyotuarifu wadau hao wasio wa kiserikali walilalamikia kile wanachokidai kuwa kudhibitiwa kwa haki za binadamu kama vile maafisa wa polisi kutumia nguvu kupita kiasi wanapokabiliana na waandamanaji.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive