- 230 viewsDuration: 1:29Mvutano kati ya Chama cha wahadhiri UASU na serikali umeelekezwa tena mahakamani, baada ya kikao cha kutafuta suluhu kusambaratika huku mgomo wa wahadhiri ukiingia wiki ya nne. Katibu Mkuu wa UASU, ameilaumu wizara ya Elimu kwa kukwamisha mazungumzo kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa mwaka wa 2017–2021. UASU inadai kuwa maafisa wa serikali walikwamisha mchakato huo, huku Wizara ikisisitiza kuwa fedha zinazotajwa na wahadhiri zimezidishwa na kwamba mgomo wenyewe ni haramu.