Vijana wanaoishi mijini wanakabiliwa na hatari zaidi ya kudhulumiwa na kuuawa na polisi

  • | K24 Video
    94 views

    Zaidi ya miaka mitano baadaye, kina mama waliowapoteza watoto wao katika njia tatanishi baada ya kupigwa risasi na polisi bado wanalilia haki zao. Vijana wanaoishi mijini sasa wanakabiliwa na hatari zaidi ya kudhulumiwa au kuuawa na polisi. Hayo ni kulingana na uchunguzi wa muungano wa vyama vya uanaharakati wa haki za kibinadamu wa missing voices. Mwaka huu watu 60 wametoweka baadhi wameaga dunia na wengine hawajulikani waliko. mumbi wambugu anaarifu zaidi.