Uhaba wa dawa katika hospitali ya Kangundo level 4 kaunti ya Machakos

  • | Citizen TV
    210 views

    Wagonjwa wanaotafuta huduma za matibabu katika hospitali ya Kangundo level 4 kaunti ya Machakos sasa wanalazimika kutafuta sehemu mbadala kununua dawa kufuatia uhaba kwenye hospitali hii

    Wagonjwa pia wanasema kuwa wanakosa huduma muhimu kama vile maji katika hospitali hii ya umma. Ni hali iliyowalazimu baadhi ya viongozi kufika eneo hilo kujaribu kutafuta suluhu. Seneta wa Machakos Agnes Kavindu akiwataka wasimamizi wa hospitali kuwajibika kuhakikisha changamoto za wagonjwa zinashughulikiwa ikiwemo hata huduma za ambulensi. Hata hivyo, usimamizi wa hospitali umekanusha madai haya.