Kizaazaa chashuhudiwa mahakamani Milimani baada ya wanaharakati kutatiza shughuli

  • | K24 Video
    113 views

    Kizaazaa kilishuhudiwa katika mahakama ya Milimani baada ya wanaharakati kutatiza shughuli na kulazimisha jaji kuondoka mahakamani. Wanaharakati walitamaushwa na hatua ya kaimu inspekta jenerali wa polisi Gilbert Masengeli ya kukiuka agizo la mahakama na kukosa kuhudhuria vikao vya mahakama kwa mara ya nne sasa kujibu sintofahamu ya waliko watu watu waliotekwa nyara Kitengela. Mahakama inatarajia mkuu huyo wa polisi kujiwasilisha Jumatatu baada ya kudai kuwa yuko Mombasa kikazi.