Wanaharakati watetea haki za mtoto wa kiume Kajiado

  • | Citizen TV
    243 views

    Wanaharakati wa kuwatetea watoto nchini wameeleza wasiwasi wao kuhusu namna juhudi zote za kuwatetea watoto zinaendelea kuelekezwa kwa watoto wasichana huku wenzao wa kiume wakitelekezwa na kuwachwa kupambana na ulimwengu. Wakizunguza kwenye hafla ya Kina mama kwenye shule moja huko Kajiado wanasema sasa kuna haja ya juhudi pia kuwekwa kuwatetea na kuwaonyesha njia ya maisha watoto wavulana ili kuwepo na usawa katika siku za usoni.