Wawakilishi wadi 37 waunga mkono hoja ya kumtimua Gavana wa Kericho Eric Mutai

  • | Citizen TV
    249 views

    Hoja iliyowasilishwa jana katika bunge la kaunti ya Kericho ya kumuondoa Gavana Eric Mutai imeungwa mkono na wawakilishi wadi 37. Mwakilishi wadi ya Sigowet, Kiprotich Rogony anadai kwenye hoja hiyo kwamba Gavana Mutai amekiuka katiba, sheria mbalimbali za kitaifa na kaunti, matumizi mabaya ya ofisi na utovu mkubwa wa nidhamu. Madai hayo yanajumuisha kushindwa kwake kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria na kutozingatia kanuni za usimamizi wa fedha za umma. Mwakilishi huyo ameeleza kwamba Gavana Mutai amekiuka katiba kwa Matumizi mabaya ya fedha za umma huku akidai kuwa ofisi ya gavana imekuwa ikitumia vibaya fedha zilizotengewa miradi ya maendeleo. Gavana Erick Mutai amepewa siku saba kujiandaa kwa utetezi wake kufuatia ilani ya kumwondoa madarakani.