Skip to main content
Skip to main content

Shughuli ya kutazama mwili wa Raila Odinga bungeni yasitishwa baada ya umati kuvamia eneo hilo.

  • | Citizen TV
    3,405 views
    Duration: 2:36
    Shughuli ya Kuutazama Mwili wa marehemu Raila Odinga iliyokuwa imepangwa kufanyika katika majengo ya Bunge ilisitishwa mapema leo, baada ya umati mkubwa wa waombolezaji kujitokeza. Umati huu wa wakenya ukionekana kupuuza taratibu za kusubiri kutazama mwili huo na kujaribu kuingia bungeni kwa nguvu. Ilichukua juhudi za Mbunge wa Embakasi East Babu Owino, kuwatuliza vijana hao waliokuwa wakitishia kuvamia majengo ya Bunge