EACC yashinikiza ushirikiano kukomesha ufisadi

  • | Citizen TV
    76 views

    Kufanikisha vita dhidi ya ufisadi nchini kutachukua muda mrefu iwapo vita hivyo vitaachiwa tume ya maadili na kupambana na ufisadi pekee. Haya ni kwa mujibu wa naibu mkurugenzi wa elimu na hamasa ya umma wa eacc Emily Mworia. Wakizungumza mjini machakos wakati wa ufunguzi wa warsha ya wakaguzi wa bajeti na wafanyakazi wa serikali, maafisa wa Eacc wameeleza umuhimu wa ushirikiano baina ya wadau mbalimbali kufanikisha vita dhidi ya ufisadi. eacc inasema kuwa ukosefu wa ushirikiano unalemaza juhudi za EACC kukabiliana na ufisadi nchini. utoaji wa habari kuhusu ufisadi katika mashirika ya serikali na ulinzi wa wanaofichua ushahidi ni changamoto kuu.