Viongozi wa makanisa waonya kuhusu mihemko ya kisiasa inayoendelea

  • | Citizen TV
    737 views

    Viongozi wa makanisa sasa wanasema kuwa kivumbi cha siasa kinachoendelea dhidi ya naibu rais Rigathi Gachagua ni njama ya kuwabadili mkondo wakenya kwa maswala muhimu yanayoendelea. Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Jackson Ole Sapit akisema kwamba, wakenya wanafungwa macho kuzima sakata ya kandarasi ya Adani na hata maswala yanayohusu bima mpya ya afya.