Kampuni ya Safaricom yatoa msaada kwa shule ya walemavu Vihiga

  • | Citizen TV
    225 views

    Serikali imetakiwa kuwekeza zaidi katika elimu ya watu wanaoishi na ulemavu ili kuwapa nafasi sawa kupata elimu. Wadau mbalimbali wametoa wito huu huku Naibu kamishina wa kaunti ya Vihiga akilalamikia idadi ndogo ya wanafunzi kutokana na hulka ya wazazi kuwaficha wana wao wanaoishi na ulemavu. Na kama anavyoarifu laura Otieno, wakfu wa Safaricom umetoa ufadhili wa shilingi milioni hamsini kuimarisha miundombinu katika shule moja huko Vihiga ya wanaoishi na ulemavu wa kusikia.