Waathiriwa wa mafuriko Tana River wanateta

  • | Citizen TV
    135 views

    Waathiriwa wa mafuriko katika kaunti ya Tana River sasa wanataka serikali ya kaunti hiyo kuharakisha mpango wa kuwapa vifaa vya kujenga makazi mapya wakisema wanapitia changamoto nyingi za kimaisha. serikali ya kaunti hiyo inanuia kuwahamisha wenyeji wa vijiji vya Mororo, Ziwani na Bakuyu kutoka eneo lililofurika na kuwapa makao ya kudumu na salama katika sehemu iliyotengwa. Waathiriwa hao ambao wamehamia sehemu hiyo wanalalamika kukosa huduma na bidhaa muhimu kutoka kwa serikali na kutaka idara husika kuharakisha utoaji wa huduma hizo.