- 14,375 viewsDuration: 4:38Familia za waliopigwa risasi wakati wa mvutano na maafisa wa polisi uliotokea katika uwanja wa Moi International Sports Center Kasarani Alhamisi wanadai haki itendeke. Vincent Otieno Ogutu na Evans Kiche, ni miongoni mwa watu watatu ambao kufikia sasa wameripotiwa kufariki. Familia zao zinasisitizia kuwa mapenzi yao kwa aliyekuwa waziri mkuu hayati Raila Odinga hayakuwa hatia wala sababu ya kuuwawa kwao.