- 12,323 viewsDuration: 4:18Mama Ida Odinga amewarai wananchi kuzingatia amani wakati wa shughuli za mazishi ya Hayati Raila Odinga. Akizungumza nyumbani kwake Opoda Farm, huko Bondo, Siaya, Mama Ida alishukuru kw ajumbe nyingi za rambirambi kutoka kwa watu mbalimbali humu nchini na kimataifa. Mama Idah aliwarai wakenya kutofanya fujo wakati wa hafla ya maombolezo na mazishi, akisema kuwa mumewe, marehemu Raila Odinga alikuwa mpenda amani.