7,103 views
Duration: 4:18
Kifo cha aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga kimefufua kumbukumbu za maisha yake ya utotoni katika mtaa wa Jerusalem eneo la Eastlands Nairobi ambapo babake, Jaramogi Oginga Odinga, aliishi kabla ya kenya kujinyakulia Uhuru. Wakazi wanamkumbuka kwa upendo Raila alipokuwa mdogo akikulia katika eneo hilo linalojulikana zaidi kama “Kwa Odinga.” Mnamo miaka ya 60 mzee Jaramogi,alihamisha familia yake hadi mtaa wa Lavington, nyota yake ya kisiasa ilipozidi kung’aa na kuteuliwa makamu wa kwanza wa rais.