Aegis Football Academy yaandaa mashindano ya kusaka vipaji mtaani Zimmerman

  • | Citizen TV
    574 views

    Kituo cha soka cha AEGIS Football Academy jijini Nairobi kimeandaa mashindano ya hisani mtaani Zimmerman, Kaunti ya Nairobi. Mashindano hayo yanalenga kutafuta na kukuza vipaji miongoni mwa wachezaji wachanga wenye umri wa kati ya miaka 7 na 11. mwanzilishi wa kituo hicho cha Aegis, Veer Dave anasema mpango huo unalenga kubadilisha mustakabali wa vijana wenye vipaji ambao wanakuwa kwenye mazingira duni.