
92 views
Katika Kitengo cha Jasho Langu, Riziki Yangu, ambacho hukujia kila Siku ya Jumanne saa moja asubuhi; Leo tunaelekea katika eneo la Taveta, katika Kaunti ya Taita Taveta ambapo nyuma ya ukimya wa mashamba, kuna wanawake wanaojikakamua kuzilisha familia zao. Tunawangazia wanawake wazee wakiongozwa na Zainati Hajji, ambao, licha ya umri wao, bado wanajitosa shambani kwa bidii wakilima ili kujikimu kimaisha. Lengo lao si tu kujilisha bali pia kuwalea na kuwasomesha wajukuu wao, wakiepuka utegemezi na usumbufu kutoka kwa wengine. Edited & Uploaded by Razaq Malik Graphics by John Muthui ©2025 Radio47 Cape Media Limited